IQNA

Jinai za Wazayuni

Hamas yahimiza kuundwa kwa Muungano dhidi ya Uvamizi wa Israel

17:06 - August 15, 2022
Habari ID: 3475627
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas imetoa wito wa kuundwa muungano dhidi ya vitendo vya uchokozi vya utawala wa Kizayuni wa Israel, baada ya takriban wanajeshi watatu wa Syria kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Israel dhidi ya Syria.

Hazem Qassem, msemaji wa Hamas, alisema katika taarifa yake kwamba " utawala wa Kizayuni na  kigaidi" umepanua uchokozi wake dhidi ya Wapalestina kufuatia wimbi la hivi karibuni la mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza, mauaji ya kukusudia ya raia, operesheni za mauaji katika Ukingo wa Magharibi. , na uvamizi katika Msikiti wa al-Aqswa mjini Quds (Jerusalem).

Qassem ameongeza kuwa, utawala wa Israel sasa umeendeleza  uchokozi kupitia mashambulizi ya kikatili ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria.

Amesisitiza kuwa, ugaidi unaoendelea na kupanuliwa wa Wazayuni katika eneo la Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) lazima ukabiliwe kwa njia ya misimamo ya pamoja ya nguvu zote ndani ya ulimwengu wa Kiislamu.

"Mataifa ya kikanda yanapaswa kusimama dhidi ya serikali na kukomesha uhalifu kama huo," Qassem alisema.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA lilisema Jumapili kwamba mashambulizi ya makombora ya Israel yalifanyika saa mbili usiku na kulenga "baadhi ya maeneo" mashambani karibu na mji mkuu, Damascus, na mkoa wa pwani wa Tartous.

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria vilikabiliana na uchokozi huo wa utawala wa Kizayuni kwa kutungua kuangusha baadhi ya makombora, SANA iliripoti, ikinukuu chanzo cha kijeshi ambacho hakikutajwa jina.

"Uchokozi huo ulisababisha vifo vya wanajeshi watatu na kujeruhiwa kwa wengine watatu," iliongeza.

Mashambulizi ya Damascus yalifanywa kutoka upande wa kusini mashariki mwa Beirut, wakati mashambulizi ya Tartous yalitoka Bahari ya Mediterania.

Syria imekuwa ikikabiliwa na hujuma za magaidi na wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni tangu Machi 2011. Serikali ya Syria imesema utawala wa Israel na washirika wake wa Magharibi na kieneo wanayasaidia makundi ya kigaidi ya kitakfiri ambayo yanaendelea kuleta uharibifu nchini humo.

Israel mara nyingi hulenga maeneo ya kijeshi ndani ya Syria, hususan yale ya harakati ya mapambano ya Lebanon ya Hizbullah ambayo imekuwa na nafasi muhimu katika kulisaidia jeshi la Syria katika mapambano yake dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni.

Israel imekuwa mmoja wa wafuasi wakuu wa makundi ya kigaidi yanayopinga serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Rais Bashar al-Assad tangu wapiganaji wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni kulipuka nchini Syria.

3480109

captcha