IQNA

Kaaba Tukufu

Viongozi Saudia washiriki katika kuosha Kaaba Tukufu

17:25 - August 16, 2022
Habari ID: 3475630
TEHRAN (IQNA) – Maafisa kadhaa wa Saudia walihudhuria sherehe za kila mwaka za kuosha Kaaba Tukufu katika mji wa Makka Jumanne asubuhi.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mwanamfalme na Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman, ambaye pia ni naibu waziri mkuu na waziri wake wa ulinzi wa ufalme huo.

Baada ya kuwasili katika Msikiti Mkuu, Mwana Mfalme, akifuatana na Waziri wa Michezo Mwanamfalme Abdulaziz bin Turki, alipokelewa na Sheikh Abdulrahman Al-Sudais, Mkuu wa Urais wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina.

Alifanya tawaf (kuizunguka Kaaba Tukufu) na akasali rakaa mbili za sala ya Sunna. Baada ya hapo, alielekea ndani ya Al-Kaaba, ambako aliongoza zoezo la  kuosha na kisha akasali rakaa mbili.

Waliohudhuria sherehe ya kuosha ni pamoja na Gavana wa Taif Prince Saud bin Nahar bin Saud; Gavana wa Jeddah Prince Saud bin Abdullah bin Jalawi; na idadi ya wajumbe wa Baraza la Wanachuoni wa Ngazi za Juu, akiwemo Sheikh Saleh bin Abdullah bin Humaid, Sheikh Abdullah bin Muhammad Al-Mutlaq, Sheikh Saad bin Nasser Al-Shathri, na Sheikh Bandar bin Abdulaziz Balila, na mtumishi mkuu wa Al-Kaaba.

Uoshaji wa kila mwaka wa eneto  takatifu zaidi la Kiislamu ulifanyika kwa kutumia maji ya Zamzam yaliyochanganywa na maji ya waridi, udi na manukato mengine.

Kuoshwa kwa Al-Kaaba Tukufu kila mwaka kumetajwa kuwa ni katika kufuata  mfano uliowekwa na Mtume Muhammad SAW.

3480115

captcha