IQNA

Ugaidi Afrika

Magaidi wa Daesh waua zaidi wa watu 30 katika hujuma kaskazini mwa Mali

16:53 - September 11, 2022
Habari ID: 3475764
TEHRAN (IQNA)- Shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh kaskazini mwa Mali limesababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Mali, nchi maskini isiyo na mipaka ya maji, imekuwa ikipambana na makundi ya kigaidi kwa muongo mmoja, na vikwazo vimedhoofisha sana uchumi wa nchi hiyo.

Taarifa zinasema, zaidi ya raia 30 wameuawa katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) huko Talatay, kilomita 150 kutoka mji wa Gao, kaskazini mwa Mali.

Mapema mwaka huu wa 2022, takriban raia 40 waliuawa katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la ISIS kwenye eneo la Tessit nchini Mali.

Hapo awali Umoja wa Mataifa ulitangaza katika ripoti yake kwamba zaidi ya raia 500 waliuawa katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo nchini Mali kati ya Januari na Machi 2022.

Takwimu hizi zinaonyesha ongezeko la asilimia 324 la mauaji ya raia ikilinganishwa na miezi mitatu iliyopita na vilevile kushindwa kwa serikali ya kijeshi ya Mali kupunguza ukiukwaji wa haki za binadamu au kukabiliana na vitendo vya ukatili vya makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Daesh katika nchi hiyo.

Tangu mwaka 2012, Mali imekumbwa na mzozo na matatizo ya kiusalama, na vikosi vya majeshi ya kigeni havijaweza kurejesha usalama nchini humo.

3480423

Kishikizo: mali ugaidi al qaeda
captcha