IQNA

Kuhifadhi Qur'ani

Mvulana Mfilipino mwenye umri wa miaka mitano ahifadhi Qur'ani kikamilifu

17:31 - September 11, 2022
Habari ID: 3475766
TEHRAN (IQNA) – Mtoto wa miaka mitano wa Ufilipino ameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamiliofu katika kumbukumbu yake.

Akiwa na umri wa miaka 5, Al-Hafiz Mohammad Abdulmohaimen Campong ni  mvulana wa eneo la Bangsamoro Ufilipiono na amepata tufiki ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Mafanikio yake ya ajabu ya kuhifadhi kikamilifu Quran katika umri mdogo sana yalitangazwa na baba yake kupitia chapisho Facebook mwezi uliopita. Baba yake alikuwa mhusika mkuu katika mafanikio hayo.

Mohammad ni mtoto wa Sheikh Abdulmohaimen Abdulrahman Campong, Maguindanaon ambaye kwa sasa anapata shahada yake ya uzamili ya Lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar huko Cairo, Misri. Yeye pia ni mjukuu wa mmoja wa waanzilishi wa Harakati ya Ukombozi wa Eneo la Moro nchini Ufilipino (MNLF), Abukhalil Yahya Abdulrahman Campong Rahimahullah.

Sheikh Campong alisema kila mara alimsomea mke wake Qur'ani alipokuwa mjamzito.

"Mke wangu alipokuwa na ujauzito wake wa miezi sita waMohammad, ilikuwa ni desturi yangu kusoma Qur'ani karibu na tumbo la mama yake kabla na wakati wa kulala, na anapoamka. Hii ikawa ni kawaida hadi mke wangu alipomzaa," Campong alisema.

"Wakati alipokuwa anainukua, hakuweza kulala bila kumsikiliza mtu anayesoma Qur'ani. Alipokuwa na umri wa miaka 3, nilishangaa kujua kwamba tayari alikuwa na uwezo wa kuhifadhi Surah Al-Baqarah (sura ndefu zaidi ya Qur'ani ) na Suratul Al-Imran. Niliendelea kumfundisha kupenda na kujifunza Qur'ani kwa moyo."

Campong alisema wakati mwingine humwona mwanawe akilia wakati akisoma kitabu hicho kitakatifu.

"Nilipomuuliza kwa nini analia, alijibu tu kuwa hajui, hawezi kueleza hisia zake. Alisema anajisikia furaha na kufurahi kila anaposoma Qur'ani," alieleza.

Kuhifadhi aya zote za Qur'ani kumekuwa jambo la kawaida tangu enzi za mwanzo wa Uislamu.

Hata katika zama hizi za kidijitali, ambapo kuhifadhi kiasi kikubwa cha data kwenye kumbukumbu ni rahisi, mamilioni ya Waislamu duniani kote wanaendelea kujifunza Qur'ani kwa moyo na wameshika utamaduni huo wa kuhifadhi. Hafidh ni jina alilopewa Mwislamu ambaye ameweza kuhifadhi katika kumbukumbu yake Qur'ani Tukufu yenye sura 114 na aya 6,236 zinazojumuisha takriban maneno 80,000.

3480427

captcha