IQNA

Jukwaa la Kimataifa la Qur’ani katika Chuo Kikuu cha Al Qasimia,UAE

22:38 - September 24, 2022
Habari ID: 3475832
TEHRAN (IQNA) – Chuo Kikuu cha Al Qasimia, katika Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE), kimehitimisha duru ya kwanza la Jukwaa la Kimataifa la Qur’ani.

Jukwa hilo ambalo limefanyika chini ya maudhi ya , "Mbinu za Kufundisha Qur’ani Tukufu Katika Zama za Sasa ", lemeendelea kwa muda la siku mbili lilikuwa limeanza Alhamisi huko Sharjah.

Kikao hicho kilishughulikia mada kadhaa muhimu kuhusu Qur’aniTukufu na njia za kufundisha usomaji wa Qur’ani.

Kongamano hilo ambalo liliandaliwa na Chuo cha Qur'ani Tukufu ikiwa ni shughuli ya kwanza ya chuo hicho wakati wa kuanza kwa mwaka wa masomo wa 2022/2023, lilishughulikia mada kadhaa muhimu zinazohusiana na Qur'ani Tukufu, zikiwakilishwa ambapo zimejikita katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu, mbinu za kufundisha usomaji wa Qur'ani Tukufu, mbinu za kufundisha michoro ya Qur'ani, pamoja na mbinu za ufundishaji tafsiri  ya Qur'ani Tukufu na mbinu za kufundisha usomaji wa Qur'ani.

Jukwaa hilo, kwa mujibu wa Awwad Al Khalaf, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Al Qasimia, lilitimiza malengo kadhaa ya chuo hicho.

Chuo cha Qur'ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Al Qasimia kilichoanzishwa mwaka 2017 kikiwa chuo cha kwanza cha Qur'ani Tukufu nchini UAE, kinatafuta kupitia kongamano hili kuupa uwanja wa kisayansi utafiti muhimu na mapendekezo ya kibunifu.

3480600

captcha