Waziri wa Masuala ya Kidini Tunisia
Waziri wa Masuala ya Dini Tunisia Sheikh Uthman Batikh amesisitiza kuhusu ulazima wa kukabiliana na misimamia mikali pamoja na harakati za wakufurishaji na kuongeza kuwa, 'leo wale wenye misimamo mikali wameharibu sura ya Uislamu'.
2015 Dec 07 , 18:27
Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kwa vijana wa Magharibi ni msingi mpya wa kuamiliana ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi ambao umejengeka juu ya msingi wa mantiki, ukweli wa mambo na kuheshimiwa tamaduni.
2015 Dec 06 , 22:45
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inataka kuchangia katika utulivu na maendeleo ya eneo la Mashariki ya Kati na kuimarisha umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.
2015 Dec 06 , 10:45
Shirika la Kutoa Huduma za Satalaiti kwa Televisheni limelaaniwa kwa kuzima televisheni ya Al-Manar iliyokuwa ikirusha matangazo yako kupitia mitambo ya shirika hilo.
2015 Dec 06 , 05:26
Waislamu katika eneo la Qatif Saudi Arabia Ijumaa hii wametoa wito wa kusitishwa hukumu ya kunyongwa mwanazuoni maarufu wa Kiislamu katika eneo hilo Sheikh Nimr Baqir An Nimr.
2015 Dec 06 , 04:53
Waislamu nchini Marekani wamebainisha wasiwasi wao mkubwa kuhusu wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kufuatia mauaji yaliyofanyika California.
2015 Dec 04 , 19:38
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Gholam Ali Khoshrou amesema barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi iliwasilisha matazamo halisi wa Uislamu.
2015 Dec 04 , 19:36
Wafanyaziara takribani milioni 27 wakiwemo wageni milioni tano wameshiriki katika maombolezo ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW, Imam Hussein AS, katika mji wa Karbala nchini Iraq.
2015 Dec 04 , 19:31
Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia leo wamehuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW huku watu milioni 26 wakiripotiwa kufika Karbala, Iraq hadi sasa kwa ajili ya maombolezo hayo.
2015 Dec 02 , 20:51
Karibu watu milioni moja wameshiriki katika msafara wa kutembea kwa miguu kutoka mji wa Kaduna hadi Zaria kwa mnasaba wa Arubaini ya Imam Hussein AS katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
2015 Dec 01 , 18:52
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: 'Mantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kustawisha uhusiano na mataifa yote ya dunia."
2015 Dec 01 , 18:50
Barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa nchi za Magharibi imeakisiwa kwa wingi katika vyombo vya habari vya kigeni.
2015 Nov 30 , 19:57
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema harakati iliyojaa mahaba na imani ya watu wa nchi mbali mbali za dunia katika siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni moja kati ya ishara za Mwenyezi Mungu.
2015 Nov 30 , 19:52