IQNA

Waislamu 32 wauawa katika hujuma ya kigaidi ya ISIS msikitini Sana'a

12:56 - September 03, 2015
Habari ID: 3357626
Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limetekeleza miripuko ya mabomu kwenye msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Yemen Sana'a na kupelekea waumini wasiopungua 32 kupoteza maisha.

Wizara ya Afya ya Yemen imesema kuwa, watu takribani 100 wamejeruhiwa baada ya miripuko hiyo kutokea katika Msikiti wa al Moayyed, mjini Sana'a.
Vyombo vya habari vya kieneo vimeripoti kuwa, mripuko wa pili ulitokea baada ya watu kukimbilia ndani ya msikiti huo ili kuwasaidia wahanga wa shambulio hilo la kigaidi.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS limetangaza kuhusika na shambulio hilo la kikatili.
Mwezi Juni mwaka huu pia, gari lililokuwa limetegwa mabomu liliripuka karibu na msikiti wa Qubad al Mahdi katika Mji Mkongwe wa Sana'a na kuuwa Waislamu watatu na kuwajeruhiwa wengine saba. Kundi la kigaidi la Daesh lilitangaza kuhusika na shambulizi hilo.../mh

3357593

captcha