IQNA

Utawala wa Kiimla Bahrain wamvua uraia Ayatullah Isa Qasim

1:15 - June 21, 2016
Habari ID: 3470404
Utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa Bahrain umeendeleza ukandamizaji mkubwa kwa kumvua uraia mwanazuoni mkubwa na mashuhuri wa Kiislamu nchini humo Ayatullah Issa Ahmad Qasim.

Uamuzi huo wa ufalme wa Bahrain umelaaniwa vikali kitaifa na kimataifa ambapo watetezi wa haki za binadamu Bahrain wamesema utawala wa Aal Khalifa umevuka mistari myekundu.

Harakati ya Waunga Mkono Mapinduzi ya Februari 14 ya Bahrain imesema utawala wa Aal Khalifa umedhihirisha tena sera zake za ubaguzi wa kimadhehebu na kikaumu kwa amri ya mabwana zake yaani Marekani, Uingereza na Saudi Arabia.

Serikali ya kifalme ya Bahrain imekuwa ikitekeleza siasa za ngumi ya chuma kukandamiza harakati ya wananchi wanaodai haki zao za kimsingi. Mamia ya wanaharakati wa masuala ya kijamii na kisiasa wameswekwa jela nchini humo kwa tuhuma zisizo na msingi na wengine wamekuwa wakinyang'anywa uraia ili kuzima midomo yao.

Tangu tarehe 14 Februari mwaka 2011 Wabahrain walianzisha Mwamko wa Kiislamu na harakati ya  kudai uhuru, uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kukabidhiwa madaraka ya nchi kwa utawala wa kidemokrasia kwa msingi wa kura za wananchi.

3508909

captcha