IQNA

Amnesty yaitaka Bahrain iache kuwakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia

18:17 - September 02, 2016
Habari ID: 3470544
Shirika la kutetea haki za binadmau la Amnesty International limeutaka utawala wa Bahrain usitishe ukadamizaji Waislamu wa Kishia nchini humo.
Katika taarifa, Amnesty imelaani vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na utawala wa Bahrain dhidi ya Waislamu wa Kishia wanaopinga utawala wa Manama hususan tangu kunyang'anywa uraia Sheikh Issa Qaassim mwanazuoni mkubwa wa Bahrain mwezi Juni mwaka huu.

Taarifa hiyo imebaini kuwa kuwa, viongozi wa Bahrain wanapaswa kusitisha haraka iwezekanavyo vitendo vya kuwakandamiza raia wanaoukosoa na kuupinga utawala wa nchi hiyo.  Amnesty International imeongeza kuwa hadi kufikia sasa utawala wa Bahrain umewatia mbaroni au kuwaita na kuwahoji waandamanaji wengi na wanazuoni wa Kishia wasiopungua 60.

Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya wananchi dhidi ya utawala wa Aal Khalifa tangu mwezi Februari mwaka 2011. Wananchi wa Bahrain nwanataka marekebisho ya kisaisa, wanadai ikuwa huru, wanatka kutekelezwa uadilifu, kukomeshwa vitendo vya ubaguzi na kuingia madarakani serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, hata hivyo utawala wa Aal Khalifa siku zote umekuwa ukiwakandamiza raia, kuwaua na kuzuia maandamano ya amani ya raia hao.

3460893


captcha