IQNA

Mashindano ya Qur'ani kwa waliosilimu kufanyika Dubai

19:32 - October 21, 2016
Habari ID: 3470624
Mashindano ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa wale waliosilimu yamepangwa kufanyika mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, (Imarati).

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefadhiliwa na Taasisi ya Al Maalumat ambayo inafungamana na Taasisi ya Kutoa Misaada ya Dar al Ber.

Mashindano hayo yatawashirikisha watu ambao wameikubali dini tukufu ya Kiislamu maishani na  ambao wanapata au wamepata mafundisho ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani katika taasisi zinazofungamana na Dar al Ber kote Imarati.

Aidha waliosilimu ambao ni wafanyakazi wa idara za serikali na taasisi mbali mbali Imarati pia wanaweza kujisajili katika mashindano hayo.

Taasisi ya Al Maalumat imesema tarehe ya mwisho ya kujisajili kushiriki katika mashindano hayo ni tarehe 12 Novemba 2016.

Mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika Imarati maalumu ya waliosilimu yatakuwa na zawadi za fedha taslimu zaidi ya AED 50,000 kwa washindi wa kwanza 10 katika kila kategoria.

3539469

captcha