Mashhad, mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu, 2017
IQNA: Mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran umetangazwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO, kuwa mji mkuu wa Ulimwengu wa Kiislamu barani Asia mwaka 2017.
Uzinduzi rasmi hadhi hiyo umefanyika Jumanne na kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi 52 za Kiislamu duniani.