IQNA

Ongezeko la asilimia 1,000 la chuki dhidi ya Uislamu baada ya urais wa Trump Marekani

19:04 - April 28, 2017
Habari ID: 3470956
TEHRAN-(IQNA)-Kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 1,000 la vitendo vya huki dhidi ya dini Tukufu ya Uislamu tokea Donald Trump achukue urasi wa Marekani Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR)  baadhi ya matukio  na vitendo vya  chuki dhidi ya Uislamu huko Marekani ambavyo vimeripotiwa kufanywa na maafisa na wafanyakazi wa idara ya forodha na ile ya ulinzi wa mipaka ya nchi hiyo, vimeongezeka kwa karibu asilimia elfu moja katika wakati huu wa utawala wa Rais Donald Trump huko Marekani. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, viwanja vya ndege vya kimataifa huko Marekani ambavyo viko chini ya idara ya forodha na ile ya ulinzi wa mipaka ya nchi hiyo ni maeneo makuu ambako panajiri vitendo vya kibaguzi na utumiaji mabavu dhidi ya wahajiri wa Kiislamu. Baraza la Uhusiano wa Kiislamu la Marekani pia limetangaza kuwa vitendo vya kibaguzi na udhihirishaji wa chuki dhidi ya Waislamu vilivyoripotiwa kufanywa na maafisa na wafanyakazi wa idara tajwa huko Marekani vimeongezeka sana katika muda wa miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2017. 

Corey Saylor Mkurugenzi wa CAIR  anayehusika na udhibiti wa chuki dhidi ya Uislamu ameliambia gazeti la Independent la Uingereza kuwa, kuwa amri ya Trump inayowapiga marufuku raia wa nchi za Kiislamu kuingia Marekani ina mahusiano ya moja kwa moja na kuongezeka vitendo vya kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu. 

Dikrii ya pili iliyotangazwa na Rais Donald Trump kuhusu wahajiri ambayo inawazuia raia wa nchi sita za Kiislamu kuingia Marekani, imepingwa na majaji wa majimbo kadhaa nchini humo.  

Wataalamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguziya Trump pamoja na sera zake ni chanzo cha chuki, mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani.

Katika nchi jirani ya Canada pia, kumekuwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu huko Canada katika miezi ya hivi karibuni. Itakumbukwa kuwa Januari 30 mwaka huu, gaidi Mkristo, mfuasi wa Rais Trump wa Marekani, aliwaua Waislamu sita katika msikiti mmoja nchini Canada

3462685

captcha