IQNA

Mamillioni kuandamna duniani katika Siku ya Kimataifa ya Quds

14:45 - June 21, 2017
Habari ID: 3471029
TEHRAN (IQNA)-Mamilioni ya watu kote duniani wanatazamiwa kujitokeza kwa wingi kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo inafanyika Ijumaa kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na hayati Imamu Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwataka Waislamu kote duniani kushiriki katika maandamano ya siku hiyo ili kuonesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi za Israel huko Palestina.Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itaadhimishwa Ijumaa ijayo ya Juni 23.

Wananchi wa Iran wanatazamiwa kujiunga na watu wa maeneo mengine duniani na kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Akthari ya watu wa dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds kwa njia mbali mbali huku wakibainisha kuchukizwa kwao na utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wake wa Magharibi ambao wanahusika katika kuwakandamiza Wapalestina.

Tayari Siku ya Kimataifa ya Quds imeshafanyika katika baadhi ya maeneo ya dunia hasa nchi za Ulaya kutokana na kuwa Ijumaa huwa siku ya kazi na sherehe za Idul Fitr zinatazamiwa kufanyika Jumapili au Jumatatu.

Siku ya Jumapili mjini London Uingereza maelfu ya watu walijitokeza kuunga mkono ukombozi wa Palestina na kulaani utawala ghasibu wa Israel.

tokea Imam Khomeini MA atoe fatwa ya kufanyika Siku ya Kimatiafa ya Quds, wakaazi wa London wamekuwa wakifanya maandamano katika siku hiyo kila mwaka. Anasema Siku ya Kimataifa ya Quds sasa imebadilika na kuwa moja kati ya hafla za kudumu za kila mwaka mjini London.

3611814

captcha