IQNA

OIC yaitaka Myanmar ilinde haki za Waislamu nchini humo

13:01 - August 04, 2017
Habari ID: 3471102
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka serikali ya Myanmar kuheshimu haki za Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.

Akiwa katika safari ya siku nne nchini Bangladesh, Katibu Mkuu wa OIC Yusuf bin Ahmed Al-Othaimeenamesisitiza kuwa, serikali ya Mnanmar inapaswa kuheshimu na kutambua rasmi haki za kiraia za Waislamu wa Rohingya.

Wito huo umetolewa baada ya Mabudha wenye misimamo mikali kufanya mashambulizi mapya dhidi ya kijiji cha Kaing Gyi katika mkoa wa Rakhine na kuua Waislamu kadhaa.

Wito huo umetolewa baada ya Mabudha wenye misimamo mikali kufanya mashambulizi mapya dhidi ya kijiji cha Kaing Gyi katika mkoa wa Rakhine na kuua Waislamu kadhaa.

Tangu muongo wa 1960 serikali ya Myanmar ilianzisha mikakati kabambe ya kuwabinya na kuwashinikiza Waislamu wa jamii ya Rohingya ya nchi hiyo ili waache mashamba, nyumba na milki zao na kuondoka nchini humo. Mwaka 2012 serikali ya Myanmar ilizidisha mashinikizo ya kisiasa na kuchochea mashambulizi na mauaji ya Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu hao.

Serikali ya Mnanmar imewanyima Waislamu hao haki zote za kiraia na inasema wanapaswa kuondoka nchini humo na kwenda Bangladesh ambako inadai ndiko walikotoka. Hata hivyo madai hayo yanakadhibishwa na ukweli wa kihistoria unaothibitisha kuwa, Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakiishi nchini Myanmar hususan katika ardhi ya Arakan yaani Rakhine ya sasa kwa karne kadhaa zilizopita na walikuwa na utawala wa kifalme katika jimbo hilo. Kwa msingi huo mashinikizo na mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa Rohingya ni harakati ya kisiasa inayofanywa na mabudha kwa shabaha ya kuangamiza kizazi chao.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3463549

captcha