Hafla ya kusilimu na kutamka shahada mbili mwanasoka huyo ilifanyika Ijumaa hii katika msikiti wa Bonamoussadi huko Douala katika tukio ambalo limehudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu.
Mboma ambaye alikuwa katika timu ya taifa ya soka ya Cameroon maarufu kama Indomitable Lions katika uchukua ubingwa wa Afrika mara mbili (2000-2002) aliicheza timu hiyo mara 56 na kufunga mabao 33.
Hatua ya Mboma kuchagua Uislamu kama njia ya maisha imekuja miezi michache baada ya nyota mwingine wa soka Clarence Seedorf wa Uholanzi naye kusilimu.
Mboma mwenye umri wa miaka 51 amewahi pia kuchezea vilabu maarufu Ulaya kama vile Paris Saint Germain na ana shahad ya uzamili katika ukocha.