IQNA

Jinai za Daesh

Magaidi wa Daesh wadai kuhusika na hujuma dhidi ya kanisa DRC

19:14 - January 16, 2023
Habari ID: 3476413
TEHRAN (IQNA) - Kundi la kigaidi la Daesh (ISIL au ISIS) lilidai kuhusika na shambulio la bomu katika kanisa moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) siku ya Jumapili.

Mamlaka ilisema Jumatatu kwamba idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la Jumapili imeongezeka hadi 14.

Kundi hilo la kigaidi na chombo chake cha habari cha Aamaq kilitoa taarifa na kusema kuwa wanamgambo wake walitega kilipuzi ndani ya kanisa la Pentekoste huko Kasindi na kukilipua wakati watu walipokuwa katika ibada.

Magaidi hao walidai kuwa bomu hilo liliua watu 20. Mamlaka ya Kongo iliweka idadi ya waliofariki Jumatatu kuwa 14 na takriban 63 kujeruhiwa.

Wakati huo huo, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio hilo lililotokea mashariki mwa DRC wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa moja huko Kasindi, jimboni Kivu Kaskazini na kusisitiza haja ya kuwawajibisha wahusika wa shambulio hilo.

Sambamba na kutoa pole kwa familia zilizofiwa, watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na serikali yao amewatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa katika shambulio hilo la mlipuko kanisani.Aidha Guterres amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa kupitia Mwakilishi wake Maalumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, “utaendelea kuiunga mkono Serikali ya DRC na wananchi katika juhudi zao za kuleta amani na utulivu mashariki mwa nchi hiyo.”

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wakati wa kampeni zake za kuwania urais aliwahi kusema kuwa kundi la kigaidi la Daesh lilianzishwa na mtangulizi wake Barack Obama akishirikiana na Hilary Clinton.

3482099

Kishikizo: drc kongo isis au daesh
captcha