IQNA

Umrah

Mwongozo mpya wa Tawaf katika Msikiti Mkuu wa Makka mwezi wa Ramadhani

16:58 - March 07, 2024
Habari ID: 3478465
IQNA – Waislamu wanaotekeleza Hija ndogo Umrah ndio pekee wataruhusiwa kufanya Tawaf (kuzunguka Kaaba Tukufu) katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al-Haram, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Idara ya Usimamizi wa Harmain (Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina) umetangaza mipango muhimu ya Umrah wanaotembelea Msikiti Mkuu katika Ramadhani.

Ili kuhakikisha uzoefu mzuri kwa waumini wote, Tawaf katika eneo la chini la Kaaba itakuwa maalum kwa ajili ya wanaotekeleza ibada ya Umrah katika Mwezi huu.

Waumini wanaofika katika Msikiti Mtakatifu wa Makaa ambao hawafanyi Umrah wataweza kufikia sakafu ya juu ya Kaaba kwa ajili ya Tawaf wakati wa Ramadhani, eneo ambalo lina  nafasi ya kutosha kwa kila mtu.

Uongozi pia umekamilisha uteuzi wa maimamu (viongozi wa swala) ambao wataongoza swala maalum ya Tarawehe na Tahajjud katika kipindi chote cha Ramadhani.

3487437

Habari zinazohusiana
captcha