IQNA

Shekhe Mkuu wa Al Azhar

Shia na Sunni ni mbawa mbili za Uislamu

20:50 - February 22, 2016
Habari ID: 3470156
Sheikh Mkuu wa al Azhar amesema Shia na Suni ni mbawa mbili za Uislamu na kwamba kuna udharura wa kufanyika jitihada za kukurubisha pamoja wafuasi wa madhehebu hizo mbili.

Sheikh Ahmad Tayyib amesema hayo leo baada ya kukutana na Baraza la Waislamu katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta. Amesisitiza suala la kuwepo umoja na mshikamano kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni na kutahadharidha kuhusu hatari ya hitilafu baina ya maulama na wanazuoni katika ulimwengu wa Kiislamu.

Sheikh Mkuu wa al Azhar ametilia mkazo kuwa Shia na Suni ni mbawa mbili za Uislamu na kwamba ni jambo la dharura kukurubisha pamoja wafuasi wa madhehebu hizo mbili. Amesema ni haramu kuua Mwislamu sawa au Shia au Suni.

Sheikh Ahmad Tayyib ametahadharidha kuhusu tabia ya kuwa na taasubi na jazba za kidini kwa fikra makhsusi au kuwa na msimamo mkali katika madhehebu au kufanya jitihada za kuwatwisha na kuwalazimisha watu wengine madhehebu makhsusi ambavyo vinasababisha mivutano ya kidini. Amesema kuwa Uislamu ni dini ya rehma na inajumuisha madhehebu zote bila ya taasubi na misimamo mikali.

3477613

captcha