IQNA

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar

Malumbano ya Kimadhehebu ni kwa maslahi ya Wazayuni

11:53 - March 01, 2016
Habari ID: 3470171
Sheikh Ahmed el-Tayeb, mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar Misri amesisititza umuhimu wa kuimarisha umoja wa Waislamu na kuzuia malumbano ya kimadhehebu katika eneo.
Akizungumza na kanali ya Sky News Arabic Jumatatu, amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio pekee unaofaidi na malumbano ya kimadhehebu katika eneo.

Amesisitiza kuwa ugaidi unatokana na malumbano ya kimadhehebu na kikabila au kikaumu.

El Tayyeb amesema Al Azhar imeunda kamati maalumu kuzuia malumbano ya kimadhehebu na kikabila katika nchi za Waislamu.

Ameongeza kuwa kamati hiyo inapanga kutuma jumbe za amani katika nchi kama vile Syria, Yemen na Iraq ili kuleta maelewano baina ya pande hasimu katika nchi hizo.

Iraq, Syria na Yemen zimekuwa zikikumbwa na hujuma za kigaidi, uvamizi wa kigeni na vita vya ndani katika miaka ya hivi karibuni.

Magaidi wa Daesh au ISIS wamekuwa wakitekeleza ukatili na mauaji katika nchi kama vile Syria, Iraq na Libya.

Yemen nayo imekuwa kikabiliwa na hujuma ya Saudia na waitifaki wake kwa muda wa mwaka moja sasa ambapo watu zaidi ya 8000 wameuawa.

3479528

captcha