IQNA

Al Azhar yatoa wito tena kuhusu mazungumza ya wasomi wa Kishia na Kisunni

21:19 - March 09, 2016
Habari ID: 3470188
Sheikhe Mkuu wa Al Azhar, Ahmad Tayyeb ametoa wito wa kufanyika vikao vya pamoja vya wasomi Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni.

Sheikh Tayyib ameyasema Jumanne Machi 8 mjini Cairo wakati alipokutana na Rais Fuad Masoum wa Iraq na ujumbe alioandamana nao.

Katika kikao hicho, Shekhe Mkuu wa Al Azhar kwa mara nyingine ametoa wito wa kufanyika vikao vya pamoja baina ya maulamaa wa madhehebu za Kiislamu za Shia na Sunni. Amesema vikao hivyo vinapaswa kufanyika kwa lengo la kutangaza fatwa wa kuharamishwa kuuana Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni. Aidha amesema vikao kama hivyo vinaweza kuandaa mazingira ya kuzuia malumbano baina ya Waislamu duniani.

Shekhe mkuu wa Al Azhar aliongeza kuwa Iraq ni nchi kubwa ya Kiislamu na Kiarabu ambayo ina mvuto maalumu kwa kila Mwarabu na Mwislamu.

Aidha alisema Al Azhar iko tayari kuwaunga mkono kuhitimisha malumbano ya kimadhehbu nchini humo.

3481937

captcha