IQNA

Waislamu Nigeria wahimizwa kuzingatia nafasi ya msikiti katika jamii

15:39 - May 04, 2016
Habari ID: 3470291
Mwanazuoni wa Kiislamu nchini Nigeria Dr Abdullateef Abdulhakeem ametoa wito kwa Waislamu kuzingatia zaidi msikiti si tu kama sehemu ya kusimamisha sala bali pia kituo cha kurekebisha jamii.

Dr Abdullateef Abdulhakeem ambaye pia ni Kamishna wa Masuala ya Ndani katika Jimbo la Lagos ametoa kauli hiyo wakati alipohutubu katika kikao cha kumtawaza Alhaji Abdulhakeem Babatunde Huthman kuwa kiongozi wa kidini (Baba Adinni) katika mtaa wa Badagari pamoja na machifu wengine wane ambao wameteuliwa na uongozi wa Msikiti wa Badagry mjini Lagos.

Dr. Abdulhakeem amesema msikiti haupaswi kuwa sehemu ya kusimamisha sala na kusomesh dini tu bali kituo cha kuleta mabadiko mema katika jamii.

Ameongeza kuwa: "Leo watu wengi jujenga majumba ya kifahari lakini wanapuuza au wanazingatia kidogo tu ujenzi au ukarabati wa msikit, ambeo ni kituo cha harakati za kisiasa, kituo cha elimu na kituovu cha maisha ya jamii. Kwa nini watu wafumbie macho ustawi wa misikiti?"

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu Lagos amesisitiza kuwa kamati za misikiti zinappaswa kuweka mipango maalumu ya kuwezesha misikiti kutenda kazi ipasavyo na pasina kuwepo vizingiti na pia kwa kuwaheshimu viongozi wa kidini. Aidha amesisitiza kuwa kamati za misikiti zinapaswa kuhakikisha kuwa Maimamu wanaishi masiha mazuri na yenye hadhi kwani wana nafasi muhimu kama wasimamizi wakuu wa misikiti.

3494947

Kishikizo: lagos nigeria msikiti iqna
captcha