IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Utawala wa Kizayuni unalenga kuvuruga uhusiano wa Iran, Jamhuri ya Azerbaijan

8:13 - March 06, 2017
Habari ID: 3470881
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kuvuruga uhusiano mzuri wa Iran na nchi jirani ya Jamhuri ya Azerbaijan.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika mazungumzo na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan yaliyohudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani.

Ayatullah Khamenei ameashiria kukasirishwa maadui na uhusiano wa karibu uliopo kati ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan na kubainisha kwamba kati ya maadui wote, utawala khabithi wa kizayuni ndio unaofanya njama kubwa zaidi za kutaka kuudhoofisha uhusiano wa kiudugu uliopo kati ya Iran na Azerbaijan, hivyo inapasa kuwa na hadhari ya kuulinda uhusiano huo wa kiupendo uliopo. Aidha amesema, kuvutia uungaji mkono na kuwategemea wananchi ndio wenzo muhimu zaidi wa kuupa kinga utawala ya kukabiliana na madola ajinabi na akasisitiza kwamba: Kheri na maslaha ya serikali ya Azerbaijan yatapatikana kwa kwenda sambamba na hisia na mapenzi ya kidini ya wananchi hao.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa madhehebu moja ni sababu muhimu zaidi ya kuwepo ukuruba na ujamaa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wananchi na viongozi wa Jamhuri ya Azerbaijan.

Huku akiashiria kwamba Jamhuri Azerbaijan imekuwa na misimamo mizuri kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ukiwemo wa kipindi cha mazungumzo ya nyuklia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Jamhuri ya Azerbaijan daima imekuwa pamoja na Iran katika duru na nyuga za kisiasa; na misimamo yake hiyo chanya imezidi kuzikurubisha zaidi nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan alisema katika mazungumzo hayo kwamba uhusiano wa nchi mbili uko katika kiwango cha juu na kwamba baadhi ya njama zinazofanywa ili kuzusha hitilafu kati ya Iran na Azerbaijan hazitofika popote.

Aidha amebainisha kuwa uhusiano wa Tehran na Baku unaendelea kustawi na kwamba katika kipindi cha mwaka huu zimesainiwa hati 20 za ushirikiano baina ya nchi mbili, na kiwango cha uhusiano wa kibiashara kati ya pande mbili kimeongezeka.

3579625

captcha