IQNA

Ahadi ya Kweli

Vikao vya Qur'ani katika Haram ya Imam Ridha (AS) kuenzi operesheni ya Iran dhidi ya Israel

19:56 - April 16, 2024
Habari ID: 3478689
IQNA - Msururu wa vikao vha kusoma  Qur'ani Tukufu ambavyo vimepewa jina la "Ahadi ya Kweli" vinafanyika katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

Vikao hivyo vimeandaliwa na Kituo cha Dar-ul-Quran cha Idara Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) ambayo ni maarufu kama Astan Quds Razavi. Vikao hivyo vya Qur'ani vimepewa jina la Ahadi ya Kweli ambalo lilikuwa jina la  operesheni ya hivi karibuni ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) usiku wa kuamkia Jumapili ya lilifanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutumia silaha hizo dhidi ya malengo halisi.

Operesheni ya mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi, yaliyopewa jina la Ahadi ya Kweli ilisababisha uharibifu mkubwa katika kambi za kijeshi za Israel katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu. Operesheni hiyo ilikuwa ni ya kulipiza kisasi shambulio la utawala wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kusababisha mauaji ya shahidi. ya wanachama saba wa IRGC mnamo Aprili 1.

Baadhi ya maqari wa Iran wanaotambulika kimataifa, wakiwemo Mohammad Javad Panahi, Hamid Reza Ahmadivafa, Seyed Javad Hosseini, Ali Reza Rezaei na Mokhtar Dehqan wanasoma Qur'ani Tukufu kwenye vikao hivyo.

Pia wakati wa vikao hivyo, Hujjatul-Islam Abavi Sani, mtaalamu wa masuala ya kisiasa, anaelezea kuhusu vipengele tofauti vya operesheni ya kihistoria ya IRGC na matokeo yake kuhusu maendeleo katika eneo hilo.

3487946

 

captcha