IQNA

Misikiti 30,000 Iran yaanzisha harakati maalumu ya kusoma Qur'ani Tukufu

10:48 - March 07, 2017
Habari ID: 3470883
IQNA-Karibu misikiti 30,000 katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanzisha harakati maalumu ya kusoma Qur'ani Tukufu iliyopewa jina la 'Tilawat

Kwa mujibu wa Mohammad Ridha Ja'afari, Mkuu wa Elimu na Utafiti katika Kamati ya Kitaifa ya Misikiti na Vituo vya Utamaduni na Sanaa, katika harakati hiyo, nakala 800,000 za Qur'ani Tukufu zimetumwa katika misikiti husika kwa ajili ya utekelezwaji mapngo huo.

Ameongeza kuwa, mbali na tilawa au kusoma Qur'ani, misikiti 7,000 kati ya hiyo pia itakuwa na mpango ziada wa tafsiri ya aya zilizosomwa. Amesema Tafsiri ya Hamrah itatumika katika mpango huo.

Bw. Ja'afari amesema Kamati ya Kitaifa ya Misikiti na Vituo vya Utamaduni na Sanaa pia ina imeandaa harakati kadhaa za kidini, kiutamaduni na kisanaa katika misikiti kwa lengo la kuwahimiza na kuwakurubisha vijana zaidi na Uislamu.

3581528


captcha