IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Iran kuanza Aprili 19

20:56 - April 12, 2017
Habari ID: 3470932
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamepangwa kuanza tarehe 19 Aprili mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA ambapo kutakuwa na kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur'ani.

Halikadhalika pembizoni mwa mashindano hayo kutakuwa na mashindano mengine ya Qur'ani maalumu kwa wale wenye ulemavu wa macho.

Mwezi huu wa Aprili pia Iran itakuwa mwenyeji wa mashindano mengine ya kimataifa ya Qur'ani yakiwemo yale ya wanafunzi wa shule yatakayofanyika Aprili 22 na yale ya wanawake yatakayofanyika Aprili 23.

Siku chache zilizopita Hujjatul Islam Sayyed Mustafa Husseini Mkuu wa Masuala ya Qur’ani katika Shirika la Awqaf la Iran ambalo linaandaa mashindano hayo ya Qur’ani alimwambia mwandishi wa IQNA kuwa, hadi sasa washiriki 283 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano matano mbali mbali ya kimataifa ya Qur’ani nchini Iran mwaka huu.

Alisema kwa kuzingatia watakaoandamana na washiriki pamoja na wageni waalikwa, kwa ujumla wageni wa nchi za kigeni watakaoshiriki katika mashindano hayo nchini Iran wanatazamiwa kufika 400.

3462558

captcha