IQNA

Televisheni ya Kiislamu yafunguliwa kwa mara ya kwanza Malawi

16:34 - May 29, 2017
Habari ID: 3471000
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Malawi wameanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuzinduliwa televisheni ya kwanza ya Kiislamu nchini humo.

Televisheni hiyo ilianza kurusha matangazo baada ya Sala ya Ijumaa tarehe 26 Mei na hivyo kuwapa Waislamu wa nchi hiyo fursa ya kutizama vipindi vya Kiislamu pasina malipo.

Mkuregenzi wa televisheni hiyo Abdullah Omar Mdala anasema kituo hicho cha televisheni ni cha kwanza cha aina yake nchini humo. Amesema stesheni hiyo ijulikanayo kama TV Islam (TVI) itakuwa na vipindi vya kiuchumi, kiutamaduni, na kijamii kwa mtazamo wa Kiislamu. " Anasema TV Islam, ambayo nara na kuali mbi yake ni "Haki Itadumu", pia itakuwa ujumbe wa matumaini na vipindi kuhusu Uislamu, demokrasia, afya n.k.

Waislamu wa Malawi wamekuwa wakitegemea kanali za televisheni za Kiislamu kutoka nchi za kigeni ambazo wakati mwingine haziwezi kukidhi mahitaji ya Waislamu nchini humo.

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Malawi ambao Waislamu wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 30 ya watu wote milioni 17 nchini humo. Mdala anasema kwa sasa wanatarajia kuwafikia asilimia 30 ya Waislamu nchini humo na asilimia 20 ya watu wasiokuwa Waislamu.

Gideon Munthali Mkurugenzi wa Habari katika Wiara ya Habari, Mawasiliano na Teknoloajia nchini Malawi ameelezea matumaini kuwa TV Islam itaweza kutekeelza jukumu la kueneza ujumbe wa mapenzi na umoja miongoni mwa watu wote wa Malawi.

3603412

captcha