IQNA

Nakala nadra za kale za Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Sayyida Zainab SA mjini Cairo+PICHA

9:40 - January 26, 2018
Habari ID: 3471372
TEHRAN (IQNA)-Nakala nne nadra za Qur'ani Tukufu ni kati ya turathi zenye thamani katika maktaba ya Msikiti wa Sayyida Zainab mjini Cairo, Misri.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kati ya nakala hizo za Qur'ani kuna ile inayonasibishwa na Imam Ali AS na kunai le inayojulikana kama Msahafu wa Othman.

Msahafu unaonaisbishwa na Imam Ali AS una kurasa 504 na umeandikwa kwa herufi sahali za Kikufi. Msahafu huo unaminika kuandikwa katika karne ya kwanza Hijria (Karne ya saba Miladia). Ukurasa wake wa mwisho umeandikwa kwa herufi za Thuluth

Nao 'Msahafu wa Othman' umetajwa kuwa moja ya nakala za Qur'ani ambazo khalifa wa tatu aliamuru ziandikwe na kutumwa katika maeneo mbali mbali ya ulimwengu wa Kiislamu.

Msahafu huo una kurasa 1087 na umeandikwa kwa herufi sahali za Kikufi. Mradi wa utunzaji msahafu huo ulitekelezwa na kundi la wataalamu na kukamilika katikati yam waka 2017 katika kituo cha Dar ul Kutub nchini Misri.

Msikiti wa Sayyida Zainab umepewa jina hilo la Bibi Zainab SA, bintiye Imam Ali AS na ni kati ya misikiti ya kihistoria mjini Cairo. Msikiti wa Sayyida Zainab ni kati ya misikiti mikubwa na muhimu Zaidi katika historia ya Misri.

Nakala nadra za kale za Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Sayyida Zainab mjini Cairo+PICHA

 

Nakala nadra za kale za Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Sayyida Zainab mjini Cairo+PICHA

3685187

 

captcha