IQNA

Turathi

Msikiti wa Sayeda Zainab mjini Cairo umefungwa kwa muda

23:13 - February 04, 2024
Habari ID: 3478305
IQNA - Waziri wa Wakfu nchini Misri amesema Msikiti wa Sayeda Zainab huko Cairo umefungwa kwa muda ili kuharakisha kazi ya ukarabati.

Sheikh Mohammed Mukhtar Gomaa amesema katika chapisho kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, kwamba kazi ya ukarabati iko katika hatua za mwisho.

Alisema kufungwa kwa muda kwa msikiti huo ni muhimu ili mkandarasi aweze kuharakisha zoezi la ukarabati.

Msikiti huo ulifungwa Alhamisi, Februari 1, na unatarajiwa kufunguliwa tena kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, alisema.

Msikiti wa Sayeda Zainab ni msikiti wa kihistoria katika mji mkuu wa Misri na ni moja ya misikiti muhimu zaidi katika historia ya nchi hii ya kaskazini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa baadhi ya riywaya msikiti huu ni mahali alipozikwa Bibi Zainab (SA).

Hivi sasa Msikiti wa Sayeda Zainab ni mahala pa ibada na pia shughuli za Qur'ani Tukufu na mihadhara ya  kidini katika jiji.

Kazi ya mwisho ya ukarabati katika msikiti huo ilitekelezwa na wizara ya Awqaf mnamo 1969.

  4197624

Kishikizo: msikiti cairo zainab
captcha