IQNA

Mahojiano

Iran haitaingia vita vya moja kwa moja na utawala wa Israel

6:50 - April 08, 2024
Habari ID: 3478653
IQNA - Kamanda katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu haitajihusisha na vita vya moja kwa moja na utawala haramu wa Israel na kwamba jibu la shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria halitakuwa kwa  makombora na ndege zisizo na rubani pekee.

Wapinzani na maadui wa muqawama au mapambano ya Kiislamu wanajaribu kuifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iende kwa mujibu wa mpango wao lakini Iran imejiepusha na "majibu ya kimhemko," Brigedia Jenerali Hassan Rastegarpanah, Mkuu wa Mafunzo ya Upelelezi na Usalama katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein cha Iran, ameliambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) Jumapili.

Hatutaacha jinai ya hivi majuzi ya utawala wa Kizayuni iende bila majibu. Majibu yetu yatatolewa kwa wakati na mahali mwafaka," alisema.

Matamshi hayo yanajiri huku wanajeshi wa utawala wa Israel wakiwa katika hali ya tahadhari baada ya ndege za kivita za utawala huo kulenga ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus wiki iliyopita. Katika shambulio hilo washauri saba wa jeshi la Iran, wakiwemo makamanda wawili wakuu waliuawa shahidi. Maafisa wa Iran wameapa kulipia kisasi kufuatia hujuma hiyo.

"Tangu kuanza kwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa Oktoba 7 2023 hadi leo, utawala wa Kizayuni umekuwa ukitaka makabiliano ya moja kwa moja na Iran, hata hivyo, kwa kuzingatia uwezo wa kistratijia uliopo, hakuna ulazima wa kushiriki katika vita vya moja kwa moja na utawala huo." Rastegarpanah alisema.

"Lengo letu ni kuwalinda wanaodhulumiwa na kuwafichua madhalimu na kupitia diplomasia hai, tunaweza kupambana vilivyo na utawala wa Kizayuni zaidi ya matarajio ya adui," aliongeza.

"Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitaanzisha vita vya moja kwa moja na Wazayuni," alisema na kuongeza: "Rasilimali za mhimili wa mapambano, ambazo tumepewa na Mwenyezi Mungu, zitauwajibisha utawala wa Kizayuni kwa jinai zake, na hatimaye, na utawala huo utapata hasara.”

Mrengo wa muqawama una uwezo mkubwa wa kuulenga utawala wa Kizayunii kutoka Iraq, Yemen, Lebanon na Syria, aliongeza. "Kwa rehema za Mwenyezi Mungu, tunashuhudia vitendo vya kila siku vyenye ufanisi vya muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni. Kwa mfano, kulengwa kwa bandari ya Eilat kuliwashangaza Wazayuni na Wamarekani.”

Hatua za muqawama "zimehesabiwa na kwa usahihi" hadi sasa, na zitabaki hivyo kwenda mbele, alisema.

"Ni muhimu kutambua kwamba jibu letu la uchokozi wa kijeshi halikomei kwa ndege zisizo na rubani na makombora pekee," alisema, akibainisha kuwa awamu ya kwanza inahusiana na kuongeza uelewa miongoni mwa mataifa ya Kiislamu. Hatua inayofuata ni kuongeza uelewa katika jamii ya kimataifa, hususan katika nchi za Ulaya, ambako maandamano dhidi ya ukatili wa Wazayuni yameongezeka, kamanda huyo aliongeza.

Brigadier General Hassan Rastegarpanah, Head of Intelligence and Security Studies of Imam Hussein University

Hivi sasa utambulisho asili na wa kutisha ya utawala wa Kizayuni, pamoja na ukatili wake na kutojali maisha ya watoto, umefichuliwa kwa wote duniani, alisisitiza.

Haya ni matokeo ya moja kwa moja ya muqawama au mapambano  thabiti ya watu wa Gaza, na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu amewafichua waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Utawala huo unakaribia kusambaratika na unakimbilia uhalifu kama huo baada ili kujaribu kuchelewesha kuangamia kwake kusikoweza kuepukika, "alisema.

Utawala wa Israel umekuwa ukitekeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi Ukanda wa Gaza uliozingirwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita na hadi sasa umeua zaidi ya watu 33,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamewafanya takriban wakaazi wote milioni mbili na nusu wa Gaza kuyahama makazi yao huku mashirika ya kimataifa yakiwa na hofu ya baa la njaa kali katika eneo hilo.

 4208960

Kishikizo: syria iran ubalozi
captcha