IQNA

Muiraqi

Muiraqi aliyevunjia heshima Qur'ani atimuliwa Norway na kurejeshwa Uswidi

16:24 - April 13, 2024
Habari ID: 3478679
IQNA - Norway imekataa ombi la hifadhi la Salwan Momika, mkimbizi kutoka Iraq ambaye aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu mara kadhaa nchini Uswidi katika miezi iliyopita. Ripoti za awali zilieleza kuwa Momika alifariki akiwa Norway lakini imebainika kuwa ripoti hizo hazikuwa sahihi.

Maafisa wa Norway wameripotiwa kumkabidhi Momika kwa Uswidi baada ya kukataa ombi lake la ukimbizi,  tovuti ya An-Nusra iliripoti.

Aliliambia gazeti la kila siku la Uswidi la Expressen kwamba kwa kuwa kibali chake cha kuishi nchini Uswidi kitaisha Aprili 16, ataomba hifadhi nchini Uswidi tena.

Momika alikuwa ameomba hifadhi nchini Norway baada ya Uswidi kusema haitongeza muda wa kibali chake cha ukimbizi.

Alipowasili Norway mnamo Machi 28, alizuiliwa na polisi wa Norway na tangu wakati huo alikuwa amezuiliwa katika kituo cha kizuizini cha wahamiaji cha Trandum.

Idara ya usalama ya Norway ilitathmini Momika kama "tishio kwa masilahi ya kimsingi ya kitaifa," kulingana na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Oslo.

Momika, ambaye alipewa kibali cha kuishi nchini Uswidi mwaka 2021, anajulikana sana kwa vitendo vyake vya kuvuruga Qur'ani nchini humo.

Vitendo vyake nchini Uswidi na Denmark, vilivyohalalishwa chini ya kisingizio cha uhuru wa kujieleza, vimechochea hasira katika nchi za Kiislamu na kusababisha mashambulizi dhidi ya balozi.

Katika kukabiliana na maandamano yaliyoenea, Denmark ilitunga sheria mwezi Desemba mwaka jana inayoharamisha uchomaji wa hadhara wa nakala za Qur'ani. Uswidi pia inazingatia hatua za kisheria zitakazowezesha polisi kukataa vibali vya maandamano kwa misingi ya usalama wa taifa.

3487912

captcha