IQNA

Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Marseille Ufaransa

Uwahhabi ni tatizo la kubwa katika dunia ya leo

17:06 - January 18, 2016
Habari ID: 3470058
Ismail Muraymi mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Marseille Ufaransa amesisitiza kuhusu udharura wa Waislamu wa madhehebu zote na dini zote kuishi kwa pamoja kwa amani huku akibainisha kuwa, tatizo kubwa la Ulimwengu wa Kiislamu ni fikra za Kiwahabbi na ukufurishaji.

Muraymi ameyasema hayo katika mkutano wake na Sayyid Abdulamir Mousawi, mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Algeria.

Katika mkutnao huo uliofanyika afisi za Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Algiers, walijadili masuala ya utamaduni, kijamii, kielimu na hali ya Waislamu Waalgeria wanaishi Marseille kusini mwa Ufaransa.

Muraymi mwenye asili ya Algeria na ambaye sasa na mkaaza wa Ufaransa amesisitiza umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani na maelewano baina Waislamu wa madhehebu zote na pia wafuasi wa duni zinginezo za Mwenyzi Mungu. Amebainisha wazi kuwa tatizo kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu ni fikra potovu za Kiwahhabi na ukufurishaji.

Muraymi anataamiwa kuitembelea Iran mwezi ujao kwa lengo la kutathmini uwezo wa Iran aktika sekta za elimu, utamaduni na utalii.

3468377

captcha