IQNA

Televisheni ya Kiwahhabi ya Peace TV yapigwa marufuku Bangladesh

16:08 - July 11, 2016
Habari ID: 3470446
Serikali ya Bangladesh imeipiga marufuku televisheni ya satalaiti maarufu kama 'Peace TV' inayofungamana na mhubiri wa Kiwahhabi Zakir Naik kwa tuhuma za kuunga mkono misimamo mikali na ugaidi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumapili Julai 10 serikali ya Bangladesh ilitoa amri ya kusitishwa matangazo ya televisheni ya satalaiti ya Peace TV yenye makao yake Dubai. Serikali ya Bangladesh imesema televisheni za nchini humo hazina idhini tena ya kurusha matangazo ya Peace TV kutokana na kuwa televisheni hiyo inaeneze misimamo mikali ya kigini na kuhumiza harakati za kigaidi kupitia mawaidha na hotuba ambazo hutolewa na Zakir Naik, kiongozi wa Mawahhabi nchini India.

Waziri wa Habari wa Bangladesh, Hasanul Haq Inu amesema Peace TV imefungwa kufuatia kikao cha kamati ya baraza la mawaziri kuhusu sheria na utengamano. Inu ameongeza kuwa: "Peace TV inakiuka maadili ya jamii ya Waislamu, Qur'ani Tukufu, Sunnah, Hadith, Katiba ya Bangladesh, utamaduni, mila na desturi zetu."

Kamati la baraza la mawaziri Bangladesh limechukua uamuzi huo baada ya tuhuma kuwa katika mahubiri yake, Zakir Naik anachochea vitendo vya ugaidi.

Tayari Zakir Naik ameshapigwa marufuku kuingia Uingereza na Canada na Peace TV imepiga marufuku katika nchi ya Kiislamu ya Malaysia.

Kati ya washambuliaji wawili ambao waliua watu 20 Julai 1 mjini Dhaka, Bangladesh wanasemekana kuwa wafuasi wa Zakir Naik katika mitandao ya kijamii.

Aidha kuna taarifa kuwa, vijana kadhaa wa India walichochewa na hotuba za Zakir Naik na kuelekea Syria kujiunga na kundi la kigaidi la ISIS. Peace TV ilianzishwa mwaka 2006 na inarusha matangazo yake katika nchi za Asia, Ulaya, Afrika, Australia na Amerika ya Kaskazini. Ina matangazo kwa lugha za Kiurdi, Banglad, Telugu na Malayalam. Peace TV imekuwa ikieneza chuki na itikadi za kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu zigine wasiofuata pote la Uwahhabi.

3514076

captcha