IQNA

Ayatullah Makarim Shirazi

Uwahhabi uko mbali na Uislamu, Saudia ni kibaraka wa Marekani

12:14 - April 07, 2016
1
Habari ID: 3470232
Ayatullah Naser Makarim Shirazi,mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu mjini Qum nchini Iran amesema kuwa Uwahhabi uko mbali na Uislamu kwani wafuasi wa pote hilo wamepotosha Uislamu.

Akizungumza, siku ya Jumatano alipokutana na wasomuna watafiti kutoka Ufaransa katika mji mtakatifu wa Qum, ameongeza kuwa wanazuoni wa Kishia na Kisunni wanaamini kuwa pote la Uwahhabi halina uhusiano na Uislamu.

Ayatullah Makarim Shirazi amebainisha kuwa Qur’ani Tukufu ni kitabu cha nuru, mantiki , rehema na mahaba.

Ayatullah Makarim Shirazi, ameendelea kusema utawala wa Saudia ni kibaraka wa Marekani na madola ya Magharibi na ndio chimbuko la mizozo katika Mashariki ya Kati.

Kiongozi huyo wa kidini ameongeza kuwa, urafiki wa Saudia na Marekani ni kwa maslahi ya Marekani na madola ya Magharibi ili sambamba na Washington kujidhaminia mafuta kwa bei rahisi iweze pia kuiuzia silaha Saudia kwa ajili ya kuendesha vita vya niaba huko Syria, Iraq na Yemen.

Ayatullah Naser Makarim Shirazi amebainisha kwamba, hakuna asiyeelewa kwamba, Saudia ni utawala wa kidhalimu na watawala wa Aal Saud kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakifanya uharibifu katika nchi za Syria, Yemen na Iraq. Ameongeza kuwa, Saudia inafanya uharibifu huo huku ikipiga marufuku raia wake kukosoa siasa zake hizo.

Ayatullah Makarim Shirazi amesema, madola ya Magharibi si ya kuaminika kwani daima yamekuwa yakitanguliza mbele maslahi yao huku yakitumia masuala kama vile haki za binadamu, usalama wa dunia, demokrasia na taasisi za kimataifa mithili ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama wenzo wa kuyashinikiza mataifa mengine.

3486479
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
saudia wanazisaliti nchi za kiarabu kwa kyshirikiana na maerkani
captcha