IQNA

Wanawake Wabosnia walaani marufuku ya Hijabu

17:21 - February 08, 2016
1
Habari ID: 3470121
Wanawake wa Bosnia wameandamana kulaani hatua ya hivi karibuni ya kupigwa marufuku vazi la Hijabu katika mahakama za nchi hiyo.

Maandamano hayo yalifanyika Jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Sarajevo, kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa Baraza Kuu la Mahakama za Bosnia kupiga marufuku 'nembo za kidini' katika taasisi za mahakama.

Waandamanaji hao walibeba mabango yaliyokuwa na nara kama vilem "Hijabu ni Chaguo Langu la Kila Siku," "Hijabu ni Haki Yangu" na "Hijabu ni Maisha Yangu."

"Tumekusanyika hapa kupinga ubaguzi na kutengwa," alisema Samira Zunic Velagic mwandalizi wa maandamano hayo.

"Marufuku hiyo ya kuvaa Hijabu katika vyombo vya mahakama ni hujuma kali dhidi ya heshima na utambulisho wa Waislamu, ni ukiukwaji wa haki na lengo lao ni kuwanyima haki ya kufanya kazi," amesema.

Uamuzi huo pia umelaaniwa na viongozi wa Kiislamu Bosnia ambao wamesema marufuku hiyo itawaathiri vibaya majaji na wafanyakazi wengine wa sekta ya mahakama.

Waislamu ni zaidi ya asilimia 40 ya wakaazi wote milioni 3.8 nchini humo.

3473778

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Jack kaimite
0
0
Nivizuri kufanya hivyo hao wabasnia waislam maana huo ndo msimamo unaotakiwa.
captcha