Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kundi la Boko Haram katika hujuma zake za hivi karibuni limewatumia zaidi, wanawake na watoto wadogo na kwamba mbinu hii imekuwa ikifanikiwa kwa kuwa wanawake na watoto wadodo ni wepesi wa kuepuka vizuizi vya maafisa usalama sambamba na kujipenyeza kwenye mijumuiko na halaiki za watu pasina kushukiwa kuwa wahalifu.
Hii ni katika hali ambayo, Toby Lanzer, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la magharibi mwa Afrika amesema kuwa, harakati za Boko Haram zimewaweka watoto nusu milioni wa kanda hiyo katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na lishe duni.
Mwezi Aprili mwaka jana, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) lilisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Boko Haram wameongeza mara 11 idadi ya watoto wanaotumiwa kufanya hujuma za kigaidi nchini Nigeria na pia katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Nigeria.
Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa
inayotumiwa na Waislamu wengi Nigeria lina maana ya 'elimu kutoka nchi
za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu
usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza
hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.
Tokea kundi hilo lianzishe uasi mwaka 2009 hadi sasa, takribani watu
20,000 wameuawa na wengine takribani milioni mbili wamelazimika kuhama
makazi yao.