IQNA

Bin Salman kuwasaidia Wazayuni kutimiza ndoto ya kuuteka mji wa Makka

16:43 - July 03, 2017
Habari ID: 3471048
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel sasa utatimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuuteka mji mtakatifu wa Makka kupitia msaada wa Muhammad bin Salman, mrithi mpya wa kiti cha ufalme nchini humo.

Bi.Madawi al-Rasheed, mpinzani mashuhuri Msaudi ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu ameashiria kuwepo muungano wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE na kusema: "Uhusiano wa karibu wa Saudia na adui Mzayuni ni jambo ambalo sasa likwe wazi".

Ameongeza kuwa: "Hivi sasa kunaandaliwa mikakati ya kuwafanya raia wa Saudi Arabia wakubali kuwepo uhusiano wa kawaida baina ya nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel na hilo linafanyika kwa kutegemea ile kaida ya "adui wa adui wangu ni rafiki yangu". Hapa watawala wa Saudia wanakusudia kuwa, kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni adui wa utawala haramu wa Israel, basi wako tayari kushirikiana na Israel kuipiga vita Iran ambayo wanaitazama kama adui wao kwa sababu inafuata madhehebu ya Kiislamu ya Shia Ithnaashariya au Jaafariya.

Bi. Madawi al-Rasheed ameongeza kuwa, hivi sasa taasisi kadhaa za Saudia zimepewa jukumu maalumu la kuandaa raia kuikubali Israeli kama rafiki. Ameendelea kusema kuwa: "Kazi ambayo bin Salman anaifanya kwa mafanikio imepelekea adui Mzayuni kuwa na furaha tele siku hizi. Hii ni kwa sababu wamefanikiwa kujipenyeza Saudi Arabia ambayo ni nchi tajiri na ndiko kuliko kibla ya cha Waislamu."

Mpinzani huyo wa Saudia aliyeko uhamishoni London amesisitiza kuwa, tayari bendera ya Israel inapepepa mjini Riyadh na hili suala halina mjadala tena. Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa sasa umefikia ndoto yake ya muda mrefu ya kuingia katika mji wa Makka na hili linafanyika kwa msaada wa Muhammad bin Salman. Ikumbukwe kuwa utawala bandia wa Israel umekuwa ukikalia kwa mabavu ardhi za Palestina kwa zaidi ya miaka 70 sasa na tokea wakati huo umewaangamiza kwa umati malaki ya Wapalestina na kuwafanya mamilioni kuwa wakimbizi. Si tu kuwa Israel imegusubu ardhi za Palestina bali pia inakalia kwa mabavu kibla ya cha kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds.

3615011

captcha