IQNA

OIC yatoa wito wa amani Syria Mwezi wa Ramadhani

18:08 - July 01, 2014
Habari ID: 1424844
Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) zimetaka kusimamishwa mapigano huko Syria katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nabil al Arabi Katibu Mkuu wa Arab League na mwenzake Iyad Madani wa OIC wamewasilisha ombi hilo wakizitaka pande husika katika mgogoro wa Syria kusitisha mapigano kikamilifu na kuacha vitendo vyote vinavyozusha amchafuko katika msimu huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

OIC na Arab League zimezitaka pande zinazozozana huko Syria kusitisha mapigano kikamilifu ili kusimamisha umwagaji damu wa wananchi wa Syria na kuwapunguzia masaibu raia hao ili kutoa mwanya kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu kusambaza huduma muhimu kwa wananchi.

Makatibu wakuu hao pia wamezitaka nchi za kieneo na kimataifa kuunga mkono ombi  lao hilo na hivyo kuishawishi serikali ya Syria na makundi ya wanamgambo kuweka chini silaha zao katika mwezi huu mtukufu.

1423950

 

Kishikizo: syria oic ramadhani
captcha