IQNA

Israel yaendelea kuua,kuharibu msikiti na nyumba Ghaza

17:30 - July 14, 2014
Habari ID: 1429748
Utawala haramu wa Israel unaendeleza jinai zake za kinyama katika Ukanda wa Ghaza ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina wakiwemo wanawake na watoto pia utawala huo umebomoa misikiti, nyumba, na mahospitali katika eneo hilo la Palestina.

Hadi sasa Wapalestina wasiopungua 175 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 1200 kujeruhiwa katika hujuma za angani za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Ghaza ambalo liko chini ya mzingiro. Nyumba za raia wa Kipalestina 560 na misikiti imebomolewa kikamilifu katika mashambulio ya anga ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza. Mufid al Hasainah Waziri wa Ujenzi na Nyumba wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina ametangaza leo asubuhi kuwa, nyumba 560 za raia wa Palestina zimebomolewa kikamilifu katika mashambulio ya anga ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Ghaza yaliyoanza siku saba zilizopita. Mbali na kubomolewa nyumba hizo za Wapalestina, nyumba nyingine za raia hao karibu ya elfu kumi na tatu zimeharibiwa pia kwenye mashambulio hayo. Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni leo asubuhi zimeushambulia mji wa Deir al Balah katikati mwa Ukanda wa Ghaza na kuubomoa kikamilifu msikiti wa al Nour katika mji huo. Wakati huo huo Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuhusu athari za kisaikolojia na kimwili za vita vya utawala wa Kizayuni kwa watoto wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza. Unicef imetangaza kuwa watoto wa Kipalestina wasiopungua 33 wameuliwa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel huko Ghaza. Taarifa ya Unicef imeongeza kuwa vita na machafuko vinaweza kuwa na taathira hasi kwa mustakbali wa watoto na kwamba watoto wa Ukanda wa Ghaza wana matatizo mengi ya kisaikolojia na kimwili yakiwemo na kuwa na jinamizi na msongo wa mawazo kutokana na kuendelea mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo. 

1429510

captcha