IQNA

Bin Talal: Saudia inawaunga mkono magaidi wa Daesh

11:09 - October 25, 2014
Habari ID: 1463446
Tajiri maarufu wa Saudi Arabia Al Waleed bin Talal amekiri kuwa nchi hiyo ya kifalme inawasaidia magaidi wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL) ambalo linapigana dhidi ya serikali za Iraq na Syria.

Bin Talal ambaye ni kutoka familia ya kifalme ya Aal Saud ameiambia televisheni ya CNN kuwa watu ambao amewataja kuwa wenye misimamo mikali ndani ya Saudi Arabia wamekuwa wakitoa misaada ya kifedha kwa magaidi.

Walid bin Talal ambaye ni mpwa wa mfalme wa zamani wa Saudia Fahd bin Abdulaziz, hatahivyo alidai kuwa eti utawala wa Saudi Arabia sasa umeacha kutoa misaada kwa magaidi wa Daesh.

Ikumbukwe kuwa magaidi wa Daesh ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq wametenda jinai nyingi sana zikiwemo mauaji ya umati, utekaji nyara, kuwafanya wanawake watumwa, kuvunja misikiti, maeneo ya kidini na makaburi ya manabii na watu watukufu. Nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo hasa Qatar, Saudi Arabia na Uturuki ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi walioko nchini Syria na Iraq.../mh

1462963

captcha