Tovuti ya intaneti ya al Sharq imeripoti kuwa, Siku ya Jumatano Vladimir Putin aliidhinisha muswada kwa kulinda Qur'ani Tukufu, Injili, Taurati na kitabu cha Wabudha. Kwa mujibu wa muswada huo, vitabu hivyo vitakatifu havipaswi kutajwa kuwa ni vitbu vyenye misimamo mikali.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni mahakama moja huko mjini Yuzhno-Sakhalinsk mji mkuu wa mkoa wa Sakhalin Oblast nchini Russia ilitoa ilitoa hukumu na kudai tafsiri moja ya Qur'ani ni yenye misimamo jambo ambalo liliibua hasira za Waislamu eneo hilo.
Yaroslav Nilov Mkuu wa Kamati ya Duma ya Taasisi za Umma na Kidini amesema kumchukulia hatua zinazofaa kulinda na kuheshimu vitabu vitakatifu ili visivunjiwe heshima.
Ameongeza kuwa moja kati ya hatua zitakazochukuliwa ni kuitaka Mahakama kuu ya Russia kutoa tangaza la kuwataka majaji kote nchini humo kuzingatia kikamilifu heshima vya vitabu vitakatifu vya kidini na marufuku ya kuvunjia heshima vitabu vitakatifu. Kwa mujibu wa katiba ya Russia, dini rasmi nchini humo ni Ukristo wa Kiorthodox, Uislamu, Uyahudi na Ubudhha.
Kuna Waislamu takribani milioni 20 nchini Russia na wengi wanaishi katika maeneo ya Cucasia, Volga, na eneo la kati mwa nchi hiyo.../mh
3385932