Sheikul Islam Talgat Tajuddin amesema misikiti hiyo imejengwa na Waislamu nchini Russia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mwanazuoni huyo amesema idadi hiyo kubwa ya misikiti kujengwa Russia ni jambo lisilo na kifani na kuongeza kwamba idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na wakati wa rais wa zamani Boris Yelstin na mtawala wa mwisho wa Shirikisho la Sovieti Mikhail Gorbachev.
Uislamu ni dini ya pili kwa wingi wa wafuaasi nchini Russia. Waislamu ni takribani ya asilimia 15 ya idadi ya wa watu wote milioni 143 nchini humo.
Kwingineko katika matamshi yake, Sheikh Tajuddin ameleeni ugaidi wa makundi kama vile ISIS au Daesh huku akitoa wito kwa Waislamu kuungana dhidi ya makundi ya kigaidi.../