IQNA

Profesa Mkristo atimuliwa chuo kikuu Marekani kwa kuvaa hijabu

11:29 - December 19, 2015
Habari ID: 3465818
Profesa Mkristo katika Chuo Kikuu cha Kikristo huko Illinois Marekani aliyevaa hijabu kubainisha mshikamano wake na Wamarekani Waislamu wanaobaguliwa ametimuliwa chuoni hapo.

Larycia Hawkins, mhadhiri na profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Wheaton ameamua kuvaa hijabu na kusambaza picha hiyo mitandaoni chini ya anuani ya “mshikamano wa kibinadamu na Waislamu” na kubainisha kuwa wanadamu wote wametoka katika chimbuko moja. Aliongeza kuwa, kama alivyosema Papa Francis hivi karibuni, Waislamu na Wakristo ‘ni watu wa kitabu’ na huabudu Mungu moja. Baada ya hatia hiyo, Chuo Kikuu cha Wheaton kimechukua hatua ya kimsimamisha kazi Profesa Hawkins na kusema baadhi ya wahadhiri hawakuafiki matamshi ya profesa huyo kuhusu uhusiano wa Uislamu na Ukristo. Pamoja na hayo, Profesa Hawkins amesema hatatikisika na ataendelea na msimamo wake huo wa kubaguliwa Waislamu. Amesema msimamo wake unatokana na mafundisho ya Nabii Issa AS (Yesu) kuhusu kuwapenda majirani. Hawkins alianza kuvaa hijabu kazini Desemba 11 kama hatua ya kupinga tamko la Donald Trump anaywania kupata tikieti ya chama cha Republican kugombea urais Mareknai ambaye alitaka Waislamu wapigwe marufuku kuingia Mareknai kufuatia hujuma ya kigaidi ya San Bernardino California ambapo inadaiwa waliotekelza hujma hiyo wana uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.
Profesa Hawkins amesema  amevaa hijabu baada ya kushauriana na Baraza la Mahusiano ya Kiislmau Marekani CAIR ili kuhakikisha kuwa hatua yake haitawaudhi Waislamu.
Kumekuwepo na wimbi la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Marekani katika wiki za hivi karibuni. Pamoja na kuwa walioanzisha wimbi hilo wanalenga kuhakikisha Wamarekani wasio Waislamu wanauchukia Uislamu lakini kumeshuhudiwa kuongezeka idadi ya wale wanaotaka kuujua Uislamu zaidi.

3465684

captcha