Maafisa wa usalama wanasema gaidi aliyekuwa amebeba bomu hilo alijilipua katika Msikiti wa Imam Ali AS baada ya Swala ya Ijumaa.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma dhidi ya msikiti huo lakini kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh ndilo ambalo hutekeleza mashambulizi dhidi ya misikiti.
Aidha leo mjini Baghdad kumetokea mripuko wa kigaidi katika eneo la Abu Ghuraib magharibi mwa Baghdad ambapo raia moja ameuawa na wengine saba kujeruhiwa.
Jana pia kulijiri miripuko maeneo kadhaa Baghdad ambapo watu nane waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Idara ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq inasema Wairaqi 1,119 waliuawa kote Iraq katika hujuma za kigaidi mwezi uliopita wa Machi.