IQNA

Harakati ya Hamas ya Palestina yatilia mkazo uhusiano wake mzuri na Iran

15:48 - October 24, 2017
Habari ID: 3471229
TEHRAN (IQNA)-Mkuu wa masuala ya kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema kuwa, harakati hiyo ina hamu ya kustawisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga zote.

Usama Hamdan amesema hayo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na gazeti la Qudsuna hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, Iran na Hamas zina uhusiano mkubwa na imara katika masuala mengi ya kiistratijia kama vile ulimwengu wa Kiislamu, kadhia ya Palestina, muqawa wa Kiislamu na kusimama imara kukabiliana na uistikbari wa mabeberu.

Mkuu huyo wa masuala ya kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amegusia pia namna Marekani na utawala wa Kizayuni zinavyofanya njama kubwa za kuzusha fitna na kujaribu kuitenganisha Hamas na Iran kwa shabaha ya kuzusha mizozo ndani ya mhimili wa muqawama na kusisitiza kuwa, kuna baadhi ya nchi zina hamu ya kuiona Hamas inatengana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini hatua ya harakati hiyo ya kutuma ujumbe wake mjini Tehran ni uthibitisho wa wazi kwamba, Hamas kamwe haiwezi kuachana na Iran na itaendelea kuwa muitifaki wake wa kudumu.

Usama Hamdan ameongeza kuwa, mambo yanayoimarisha uhusiano wa Hamas na Iran mengi na madhubuti sana na si rahisi mashinikizo kama ya Marekani na utawala wa Kizayuni kutia doa uhusiano huo.

Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas ukiongozwa na Saleh Arouri, naibu wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo uliwasili hapa Tehran siku ya Ijumaa kwa ajili ya ziara rasmi.

3656135

Kishikizo: iqna hamas iran palestina
captcha