IQNA

Wanasayansi Bora Waislamu watunukiwa Zawadi ya Mustafa SAW nchini Iran

10:58 - November 12, 2019
Habari ID: 3472211
TEHRAN (IQNA) – Awamu ya Tatu ya Zawadi ya Mustafa SAW 2019 imetangazwa Jumatatu katika mji mkuu wa Iran, Tehran, ambapo wanasayansi watatu wa Iran na wawili kutoka Uturuki wametangazwa washindi.

Kwa mujibu taarifa wanasayansi waliopata tuzo ya Mustafa SAW 2019 ni pamoja na Ali Khadem Hossini wa Iran na Ugur Sahin wa Uturuki katika kategoria ya 'Maisha, Sayansi ya Tiba na Teknolojia.  Nao Umran S. Inan wa Uturuki, Mohammad Abdol-Ahad na Hossein Baharvand wa Iran wamepata tuzo ya Mustafa SAW 2019  katika kategoria jumla ya Sayansi na Teknolojia.  Profesa Ugur Sahin ambaye anafunza katika Chuo Kikuu cha Mainz Ujerumani amepata tuzo kutokana na kazi zake katika kuvumbua na kufanyia majaribio chanjo ya saratani. Naye Profesa  Ali Khademhosseini ambaye anafunza katika Chuo Kikuu cha UCLA nchini Marekani ametunukiwa tuzo kutokana na utafiti wake katika uga wa teknolojia ya nano. 

Kwa upande wake Profesa Umran S. Inan ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Koc Uturuki ametunukiwa tuzo kufuatia utafiti wake wa kina kuhusu anga za mbali huku Profesa Hussein Baharvand wa Taasisi ya Royan akipata tuzo baada ya mafanikio yake ya kutibu ugonjwa wa Parkinson na ugonjwa wa jicho unaojulikana kama AMD kwa kutegemea seli shina. Kwa upande wake Dakta Mohammad Abdol-Ahad wa Chuo Kikuu cha Tehran ametunukiwa tuzo kutokana na utafiti wake kuhusu mbinu mpya za kutibu saratani.

Sherehe za kuwatunuzawadi wanasayansi hao bingwa wa Waislamu zimehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Iran Anayeshughulikia Masuala ya Sayansi na Teknolojia Dtk. Sorena Sattari.

Katika kuwani tuzo ya mwaka huu, zaidi ya kazi 150 ziliwasilishwa na kufanyiwa uchunguzi na jopo la majaji 500 kutoka vyuo vikuu 200 katika nchi 35 na hatimaye washindi wakatangazwa.

Zawadi ya Mustafa SAW ni zawadi ya juu zaidi ya sayansi na teknolojia ambayo hutunukiwa wanasayansi na watafiti na watafiti bora zaidi wa nchi za Kiislamu duniani. Washindi wa Zawadi ya Mustafa SAW hupata zawadi ya nusu milioni dola pamoja na cheti.

Sherezi za kuwatangaza washindi wa Zawadi ya Mustafa SAW hufanyika katika Wiki ya Umoja wa Kiislamu nchini kama sehemu ya kuadhimisha Maulid ya Bwana Mtume Muhammad SAW.

3856261

 

captcha