IQNA

Waislamu wengi wafariki kutokanana na corona Uingereza

12:35 - April 12, 2020
Habari ID: 3472658
TEHRAN (IQNA) – Idadi kubwa ya Waislamu wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona nchini Uingereza na hilo linabainika wazi katika makaburi ya Waislamu.

Bustani inayojulikana kama Eternal Gardens, ambayo hutumika kama makaburi ya Waislamu mjini London, kwa kawaida hushudia maziko ya takribani Waislamu watano kwa wiki lakini sasa idadi hiyo imeongezeka hadi 30.

Ili kukabiliana na hali iliyojitokeza wasimamizi wa eneo hilo sasa hawachimbi kaburi kwa kila mwili bali wanachimba kaburi kubwa lenye uwezo wa kuzikwa watu 10 pamoja. Hatahivyo kila mwili unakuwa na eneo lake maalumu la kulazwa la 'mwanandani' ambayo ni sehemu ndogo inayochimbwa ndani ya kaburi kwa ajili ya kumlaza maiti kwa ubavu wake wa kulia.

Siku ya Ijumaa, watu 10 walizikwa katika mstari mmoja kwa kufuata taratibu zote za Kiislamu. Imamu wa London, Sheikh Suleiman Ghani aliongoza sala ya maiti au sala ya jeneza kwa miili hiyo.

Hadi kufikia Aprili 12, 2020, watu 78,99 walikuwa wameambukizwa corona nchini Uingereza huku wengine 9,875 wakifariki dunia. 

3471112

captcha