Katika ujumbe kupitia Twitter, Spika wa Bunge la Kuwait, Marzouq al Ghanim amesema Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah ambaye kabla ya hapo alikuwa na cheo cha Mrithi wa Kiti cha Amiri ameapishwa leo Jumatano asubuhi.
Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah, Amir wa Kuwait ambaye aliaga dunia hapo jana Jumanne tarehe 29 Septemba, alikuwa mpatanishi wa mwisho mkongwe katika eneo la Asia Magharibi.
Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah ametawala Kuwait kwa miaka 14 yaani tangu mwaka 2006 hadi wakati wa kuaga kwake hapo jana Jumanne. Katika kipindi cha uongozi wake, Kuwait imeshuhudia amani na utulivu wa ndani katika nyanja tofauti.