Sheikh Mohammad Khalaileh amesema katika taarifa siku ya Alhamisi kuwa Swala ya Ijumaa itaswaliwa kote nchini humo wiki hii.
Amesisitiza kuhusu umuhimu kwa waumini kuzingatia kanuni za kiafya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kutumia zulia au mkeka binafsi wa kuswalia na kutokaribiana wakati wa swala ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.
Misikiti ilifungwa Jordan mwezi Aprili kufuatia kuenea ugonjwa wa corona. Misikiti ilifunguliwa tena kwa swala za jamaa mwezi Juni na sasa swala ya Ijumaa itaruhusiwa kuanzia wiki hii.
Tokea ugonjwa wa corona uripotiwa mapema mwezi Machi hadi sasa, watu 169,000 wameabukizwa ugonjwa huo nchini Jordan ambapo watu 2,053 wamepoteza maisha.