IQNA

Watu wa Ghana wapokea zawadi za nalaka za Qur'ani kutoka mfadhili Jordan

18:52 - July 05, 2021
Habari ID: 3474071
TEHRAN (IQNA)- Raia mmoja wa Jordan amewatunuku watu wa Ghana nakala 1,400 za Qur'ani Tukufu.

Mohammad Salim al-Ayasira amesema misahafu ambayo amewazawadia watu wa Ghana ameikusanya kutoka maeneo mbali mbali ya Jordan.

Anasema kuwa, kwa muda wa miaka 50 amekuwa akikusanya misahafu hiyo iliyotumika na kuikarabati na watu wa Ghana ni miongoni mwa aliowatunuku zawadi hiyo.

Al-Ayasira anasema kwa ujumla, mwaka huu pekee ametuma misahafu 5,000 barani Afrika kwa msaada wa taasisi kadhaa za Jordan.

3981897

Kishikizo: jordan ghana misahafu
captcha