IQNA

Makomando wa Iran wazima uharamia wa Marekani katika Bahari ya Oman + Video

19:08 - November 03, 2021
Habari ID: 3474511
TEHRAN (IQNA)- Operesheni maalumu na iliyotekelezwa wakati mwafaka na wanajeshi shupavu wa kikosi cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limefanikiwa kuzima jaribio la uharamia na wizi wa mafuta uliosimamiwa na manuwari ya kijeshi ya Marekani katika maji ya Bahari ya Oman.

Vyombo rasmi vya habari Iran vimeripoti kuwa, mashujaa wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wamezima jaribio la operesheni ya meli ya kivita ya Marekani iliyojaribu kuiba mafuta yaliyokuwa yamepakiwa katika meli ya mafuta ya Iran. 

Meli hiyo ya kivita ya Marekani ilipora na kuchukua meli iliyokuwa imesheheni mafuta ya Iran katika Bahari ya Oman na kupakua mafuta yake na kisha kuyapakia katika meli nyingine na kuielekeza kusikojulikana. 

Hata hivyo, kikosi cha anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilitekeleza operesheni kinzani na kushusha makomando wa kikosi hicho juu ya meli hiyo na kuitwaa na baadaye kuilekeza kwenye maji ya Iran.

Jeshi la  Marekani liliifuata meli hiyo kwa kutumia helikopta na meli kadhaa za kivita, lakini limeshindwa kutokana na kuingia nguvu kubwa zaidi ya vikosi vya IRGC.

Baada ya hapo, jeshi la Marekani liliifuata meli hiyo ya mafuta kwa kutumia helikopta kadhaa na meli za kivita, lakini jaribio hili pia lilishindwa kutokana na ukakamavu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Jitihada kubwa za askari wa Marekani za kujaribu kusimamisha na kuzuia meli hiyo zimefeli na kwa sasa shehena ya mafuta iiliyokuwa imeporwa na askari wa Marekani iko katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Tizama hapa chini taswira ya video ya oparesheni hiyo ya IRGC

4010451

captcha